Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Wilders, katika kampeni yake ya uchaguzi, alitumia gazeti moja maarufu la Uholanzi na kuchapisha picha iliyokuwa na uso wa mwanamke uliogawanywa katikat sehemu mbili; sehemu ya kwanza ikimuonesha mwanamke mwenye nywele za rangi ya dhahabu na tabasamu, na sehemu nyengine ikimuonesha mwanamke mwenye uso uliojaa hasira na aliyevaa hijabu, Katika kauli za kampeni, ilisemwa: “Uchaguzi uko mikononi mwenu, siku ya kupiga kura ni nani mtakayemchagua!” Na katika maandiko yaliyomo, mara kadhaa Waislamu walitajwa kwa maneno kama “wasiopendeza” na “wa kuchukiza.”
Kitendo chake hiki cha aibu kilileta mshtuko na hasira kubwa kwa umma, na mashirika kumi na manne yakamfungulia mashtaka kutokana na matendo haya.
Hata hivyo, bado anaendelea na mienendo yake ya chuki dhidi ya Uislamu, na katika akaunti yake ya "X" ameandika: “Uislamu si mali ya Uholanzi, na wanawake wetu hawapaswi kuvaa kama Waislamu.”
Wilders hapo awali pia amewahi kuchunguzwa kisheria kwa kosa la kudhalilisha makundi mengine ya kidini.
Chanzo: NL TIMES
Maoni yako